Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa program ya kitamaduni kwa anuani isemayo “Kuendeleza kipaji cha mwalimu”, kwa baadhi ya walimu wa mkoa wa Karbala.
Mkuu wa kituo bibi Sara Hafaari amesema “Program imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ikafuatiwa na mada yenye anuani isemayo “Njia ya kupata amani ya nafsi”.
Akaongeza kuwa “Program imepambwa na kipengele cha (kutoka kwenu hadi kwenu) kimekuwa na ushiriki mzuri kwa kuuliza maswali mbalimbali, ikahitimishwa kwa mashindano ya kidini chini ya usimamizi wa bibi Ikhlasu Jawadi”.
Kituo kinaendelea kuandaa program tofauti za wasichana kwa lengo la kuwajengea uwezo katika mambo ya kitamaduni na maarifa ya Dini yao, ili kupata utulifu wa familia kwa kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s).