Kitengo cha utumishi kinaendelea na kazi ya kusafisha maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya kinafanya usafi kwenye maeneo yanayozunguka haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na njia zinazo elekea kwenye eneo hilo.

Kiongozi wa idara inayosimamia jengo tukufu Sayyid Alaa Hussein Ali amesema kuwa, Tunaendelea na kazi ya kusafisha maeneo yote yanayozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu wakati wote, tunatumia vifaa maalum kwa kazi hiyo, kazi huanzia kwenye uwanja wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Kazi ya usafi inahusisha pia sehemu za kutolea huduma ndani na nje ya uzio wa Ataba, kama vile sehemu za kutunzia vitu vya mazuwaru, viatu na sehemu zingine”.

Aidha tunasafisha Barabara zinazoelekea Atabatu Abbasiyya na maeneo ya karibu na Ataba, ili kuhakikisha maeneo yote ya Jirani yanakuwa na muonekano mzuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: