Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimeratibu ziara ya pamoja katika msikiti wa Kufa na Sahlah, kwa wageni wanaoshiriki kwenye semina ya kwanza ya kuwajengea uwezo.
Mkuu wa Markazi Muheshimiwa Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema kuwa, Uongozi wa Markazi umeandaa ratiba maalum ya kutembelea Ataba tukufu na taasisi za kisekula kwa wageni (mubalighina) kutoka nchi saba za Afrika, wanaoshiriki semina ya kuwajengea uwezo awamu ya kwanza inayosimamiwa na Atabatu Abbasiyya.
Akaongeza kuwa, “Wageni wametembelea msikiti wa Kufa na Sahlah, wamefanya ziara na ibada mbalimbali katika misikiti hiyo, aidha wamepata nafasi ya kukutana na viongozi ya misikiti hiyo na kupewa historia yake”.
Tunatarajia wageni hao watatembelea sehemu mbalimbali za kiibada na taasisi za kielimu katika mji wa Najafu ndani ya siku chache zijazo, chini ya ratiba maalum iliyoandaliwa na uongozi wa Markazi Dirasaati Afriqiyya.