Hivi karibuni maktaba ya Ummul-Banina (a.s) ya wasichana katika Atabatu Abbasiyya, imechapisha toleo la (200) la jarida la Riyadhu Zaharaa (a.s) ambalo hutolewa kila mwezi.
Nalo ni jarida la kwanza kuchapishwa na Ataba za Iraq baada ya mwaka (2003m).
Chapisho jipya linamaudhui tofauti za Fiqhi, Aqida, Qur’ani, Malezi, Utamaduni, Jamii, Afya na nyinginezo.
Aidha chapisho lina anuani tofauti (Jambo zuri ni lenye mwisho mwema, mahafali kubwa ya wahitimu (2300) nchini Iraq, ukatili kwa watoto: sababu na utatuzi wake, mtu baina ya Hasi na Chanya) na zinginezo.
Unaweza kuangalia chapisho hilo kupitia link ya jarida la Riyadhu Zaharaa (a.s) ifuatayo:
https://reyadalzahra.alkafeel.net/journal/243#/