Majmaa-Ilmi imesema: Hati ya Alkafeel imetokana na mikono ya wairaq.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imesema kuwa Hati ya Alkafeel imetokana na mikono ya wairaq.

Mkuu wa kituo cha uchapishaji wa msahafu chini ya Majmaa Shekhe Dhiyaau-Dini Zubaidi amesema “Hii ni miongoni mwa hati muhimu sana, imekuwa ikitumika katika Qur’ani tukufu toka karne ya nne hijiriyya” akasisitiza kuwa “Imeanzishwa na mikono ya wanahati wa kiiraq, akiwemo Shekhe Muhammad Bun Ali bun Muqalah, Abu Hassan Ali bun Hilali, maarufu kwa ibun Albawaab, mwanahati Yaquut Musta’swimi, aliyepewa jina la Qibla ya waandishi”.

Akaongeza kuwa “Tumenufaika na teknolojia za kisasa katika kutoa herufi kwenye maandishi ya mkono na kuziweka katika uwezekano wa kutumika kwenye program za kompyuta (word) na zinginezo, aidha kuna uwezekano wa kuiboresha na kuiendeleza zaidi kwa matumizi ya wote”.

Kituo cha uchapishaji wa msahafu kimefanya hafla kubwa ya kuitambulisha hati ya Alkafeel iliyohudhuriwa na wataalam wa hati, kwa mujibu wa maelezo ya Zubaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: