Mpiga picha Atabatu Abbasiyya amekuwa mshindi wa kwanza kwenye shindano la kimataifa.

Mpiga picha wa kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya bwana Liith Ahmadi Haadi, amekuwa mshindi wa kwanza kwenye shindano la (Mji mkuu wa Mawakibu) lililofanywa nchini Iran.

Haadi amesema kuwa, amepata nafasi ya kwanza kwenye shindano la kupiga picha za mnato liitwalo (Mji mkuu wa Mawakibu) nchini Iran, kulikuwa na jumla ya washindani (3100), picha zilizo ingia kwenye hatua ya mwisho zilikuwa (252) kutoka kwa wapiga picha wa nchi zifuatazo: Iraq, Iran, India, Pakistan na Marekani.

Akaongeza kuwa “Kulikuwa na washindi wa aina tano, ambao ni: Picha za stika, Picha za filamu, Picha za kawaida, Picha za kupiga kwa kutumia simu ganja, Video za muziki na zenye muonekano tofauti”.

Haadi amekuwa mshindi wa kwanza katika kipengele cha kupiga picha za kawaida.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: