Mkuu wa Markazi bibi Sara Hafaar amesema “Shindano lilifanywa sambamba na maombolezo ya kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili, lilidumu kwa muda wa siku nne (25 – 28/11/2023)”.
Akaongeza kuwa “Tumepiga kura ili kupata washindi watatu waliopewa zawadi”, matokeo ya kura yalikuwa kama ifutavyo:
- - Sara Swadiq Ibrahim.
- - Hauraa Najmu Abdi.
- - Kawakibu Hamza Hussein.
Akafafanuwa kuwa Kituo kimetoa muhadhara wenye anuani isemayo “Mafundisho kutokana na Maisha ya Zaharaa -a.s-”, Tumeangalia utamaduni wa kutoa kwa Zaharaa (a.s) na athari yake, namna alivyo jihifadhi sambamba na kuangazia athari yake kwa wanawake wa zama hizi.
Kituo kinafanya juhudi kubwa ya kufundisha mwenendo wa Ahlulbait (a.s) kwa wasichana kwa lengo la kulinda maadili na kuzuwia mpasuko wa familia.