Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimefanya kikao na wanafunzi wa kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Al-Ameed.
Shekhe Muhammad Kuraitwi amesema “Tumefanya kikao na wanafunzi wa kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Al-Ameed, tumetoa muhadhara kuhusu maadili kwa ujumla na mwingine kuhusu maadili ya udaktari, tumesisitiza umuhimu wa kuwa na madaktari bingwa na kwamba kazi hiyo ni wito wa kibinaadamu”.
Akaongeza kuwa “Tumewaambia wanafunzi, taasisi ya Dini na sekula zitaendelea kushirikiana daima”, akasema kuwa “Kikao kimepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi”.
Wanafunzi wameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa namna kitengo cha Dini kinavyo wajali kwa kuwasiliana nao wakati wote na kuwapa mihadhara inayowajenga kielimu.