Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza kuanza kusajili washiriki wa semina ya (Saaqi ya hukumu za Qur’ani).
Semina hiyo itaendeshwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa, itafanywa katika ofisi za Maahadi zilizopo kwenye jengo la Alqami katika eneo la Farihah katika mji wa Karbala mkabala na chuo kikuu cha Karbala.
Semina itafanywa siku ya Ijumaa na Jumamosi ya kila wiki kuanzia saa (3 – 5) asubuhi, nayo ni kwa wanaume tu, watafundishwa kwa nadhariyya na vitendo.
Unaweza kujisajili kupitia link ifuatayo: https://forms.gle/rv5wnUENZVqveLaS9