Kiongozi wa idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule Sayyid Maahir Khalidi amesema kuwa “Idara imeandaa ratiba maalum ya kupokea vijana kutoka Baghdad, inahusisha kufanya ziara katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya na makumbusho ya Alkafeel”.
Akaongeza kuwa “Ratiba hii ni sehemu ya harakati za idara ya harakati za shule ndani ya kitengo cha mahusiano ya vyuo vikuu na shule kwa lengo la kuwa karibu na wanafunzi wa shule za Iraq”.
Akaendelea kusema “Ratiba imepambwa na muhadhara kuhusu mambo Matano kwa mtu mwenye mafanikio na kuhitimishwa kwa kuwapa zawadi wasimamizi wa program”.
Mzungumzaji wa umoja wa vijana Sayyid Abbasi Yaasiri Mussawi ameishukuru Atabatu Abbasiyya kwa mapokezi mazuri waliyopewa.