Kitengo cha uboreshaji kinafanya semina kuhusu program ya Excel kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya semina ya Program ya Excel kwa watumishi wa Ataba tukufu.

Mkufunzi wa semina hiyo Sayyid Muntadhiru amesema “Kitengo kimetoa semina ya matumi ya program ya Excel kwa baadhi ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya, ili kuboresha uwezo wao”.

Akaongeza kuwa “Semina inamada tofauti, miongoni mwake ni namna ya kufanyia kazi ukurasa mkuu wa Program, taarifa zinazo ingizwa, upigaji wa hesabu ndani ya Program, matokeo ya moja kwa moja, kuunganisha mapungufu na mengineyo”.

Semina itadumu wa kuda wa siku tatu, kila siku watasoma saa tatu, ndani ya ukumbi wa Naafidhu-Albaswirah, kwenye jengo la Imamu Swadiq (a.s) lenye ofisi za vitengo vya Atabatu Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: