Kongamano linafanywa chini ya kituo cha Maraya kwa usimamizi wa Atabatu Abbasiyya, na kusaidiana na jumuiya ya Al-Ameed, Uongozi mkuu wa Masjidi Kufa, chuo kikuu cha Alkafeel, Al-Ameed, kitivo cha Adabu, idara ya Uchumi katika chuo cha Kufa na muungano wa waandishi katika mji wa Najafu.
Kongamano lina anuani isemayo (Misingi ya uangalizi wa kijamii na kupambana na ufakiri katika turathi za Imamu Ali -a.s-), kuanzia tarehe 9 – 11 Desemba/ 2023m, sawa na mwezi 24 – 26 Jamadal-Uula.
Kikao cha kwanza kimesimamiwa na Dokta Abbasi Aajil Haidari, katika kikao hicho mada tofauti zimewasilishwa na wahadhiri kutoka mikoa tofauti ya Iraq.
Kikao kimefanywa leo asubufi na kujadili mambo tofauti kuhusu kiongozi wa waumini (a.s) na uongozi wake kijamii na kisiasa, mbele ya idadi kubwa ya viongozi wa Ataba na Hauza.