Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya anaangalia maendeleo ya semina za kujenga uwezo katika mambo ya utawala.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, ametembelea semina za kuwajengea uwezo katika mambo ya uongozi zinazofanywa chini ya kitego cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Ataba tukufu.

Muheshimiwa katibu mkuu amefatana na kiongozi wa ofisi ya Sayyid Ahmadi Swafi Dokta Afdhalu Shami na wajumbe wa kamati kuu, Sayyid Liith Mussawi, Dokta Abbasi Didah Mussawi, Sayyid Jawadi Hasanawi, Sayyid Muhammad Ashqar, Sayyid Kadhim Ibadah na makamo katibu mkuu Sayyid Abbasi Mussa.

Muheshimiwa katibu mkuu amekutana na kamati ya uongozi chini ya rais wa kitengo cha uboreshaji Dokta Muhammad Hassan Jaabir na makamo wake Sayyid Ali Shimri, na kuangazia mambo yanayohitajiba sambamba na kusikiliza mambo wanayokusudia kuyafikia.

Muheshimiwa katibu mkuu ametembelea kituo cha masomo ya kisekula na kuangalia maendeleo ya semina kwa lengo la kutatua changamoto walizonazo.

Semina za kujenga uwezo zinapewa umuhimu mkubwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, kwani huongeza ufanisi wa utendaji kwa watumishi wa Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: