Ameyasema hayo alipokutana na msomi wa Dini kutoka Tunisia Sayyid Muhammad Tijani, akasikiliza maelezo yake kuhusu hali ya wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika nchi ya Tunisia na harakati zao.
Sayyid Swafi akasisitiza umuhimu wa kushikamana na mwenendo wa Mtume Muhammad na kizazi chake kitakasifu (a.s), na kuakisi mwenendo wao katika maisha sambamba na kulinda umoja wa waislamu.
Akaendelea kusema: Hakika harakati ya bwana wa mashahidi (a.s) na ushindi wake mkubwa, ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ikiwemo ziara ya Arubaini na huduma zinazotolewa kwenye ziara hiyo, ni ujumbe wa kibinaadamu na kimataifa, umefika kila sehemu ya dunia, maendeleo ya teknolojia yamesaidia sana kufikisha ujumbe huo.
Sayyid Tijani akawasilisha salamu za wapenzi wa Ahlulbait (a.s) katika nchi ya Tunisia kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya na wasimamizi wake, wanawaombea Mwenyezi Mungu awawezeshe kuendelea kuhudumia mazuwaru wa malalo takatifu, akaongea kwa ujumla kuhusu hali ya wafuasi wa Ahlulbait (a.s) Afrika kaskazini.
Tijani akasema kuwa Sayyid Swafi amehimiza umoja wa waislamu katika mazingira haya magumu, akapongeza kazi kubwa inayofanywa ya kuhudumia waumini katika nchi hizo.