Kamati inayosimamia kongamano la kuhuisha turathi za kiongozi wa waumini (a.s) awamu ya tatu, imetoa zawadi kwa baadhi ya watafiti walioshiriki katika kongamano.
Kongamano limesimamiwa na kituo cha Maraya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kushirikiana na jumuiya ya Al-Ameed, uongozi wa Masjid Kufa, chuo kikuu cha Alkafeel na Al-Ameed, kitivo cha Adabu, Uchumi na muungano wa waandishi wa Najafu.
Kongamano lilikuwa na anuani isemayo (Misingi ya usimamizi wa jamii na kupambana na ufakiri katika turathi za Imamu Ali -a.s-) kwa siku mbili, viongozi mbalimbali wamehudhuria na watafiti kutoka ndani na nje ya Iraq, limehitimishwa kwa kutoa zawadi kwa watafiti walioshiriki kwenye ratiba ya kongamano.
Jumla ya mada ishirini zimejadiliwa kwenye kongamano hilo, katika vikao vine ndani ya siku mbili, kulikuwa na vikao vya asubuhi na jioni, mada tano zimewasilishwa kwenye kila kikao, tumejadili kuhusu kupambana na ufakiri na tatizo la ukosefu wa ajira, kwa kufuata misingi ya turathi za Imamu Ali (a.s), sambamba na kuangazia siasa ya usimamizi wa jamii katika historia ya kiongozi wa waumini (a.s).