Kuhitimisha ratiba ya kongamano la kuhuisha turathi za kiongozi wa waumini (a.s) awamu ya tatu.

Ratiba ya kongamano la kielimu awamu ya tatu, linalohusu kuhuisha turathi za kiongozi wa waumini (a.s) imehitimishwa mbele ya viongozi tofauti.

Kongamano limesimamiwa na kituo cha Maraya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kushirikiana na jumuiya ya Al-Ameed, uongozi wa Masjid Kufa, chuo kikuu cha Alkafeel na Al-Ameed, kitivo cha Adabu, Uchumi na muungano wa waandishi wa Najafu.

Kongamalo limefanywa chini ya anuani isemayo (Misingi ya kusimamia jamii na kupambana na ufakiri katika turathi za Imamu Ali -a.s-) kuanzia tarehe (9 – 11 Desemba/ sawa na 24 – 26 Jamadal-Uula 1445m.

Jumla ya mada (20) zimejadiliwa kwenye kongamano hilo katika vikao vinne, kutoka mada (50) zilizo wasilishwa, mada zote zimejikita katika maudhui ya malezi ya jamii, kuishi kwa amani na kupambana na ufakiri kwa kufuata msingi wa mwenendo wa Imamu Ali (a.s).

Hafla ya kufunga kongamano imeshuhudia ugawaji wa zawadi kwa wasomi waliowasilisha tafiti zao kutoka ndani na nje ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: