Sayyid Swafi amepongeza kazi ya uchoraji na katoa wito wa kufanywa kongamano la kimataifa kuhusu fani hiyo.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Sayyid Ahmadi Swafi, amepongeza kazi ya uchoraji iliyofanywa na Atabatu Abbasiyya, na ametoa wito wa kufanyika kwa kongamano la kimataifa kuhusu fani hiyo.

Ameyasema hayo alipokutana na watumishi wa kituo cha uchoraji na maandishi kwenye kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, akasikiliza maelezo kuhusu kazi yao ya uchoraji, ikiwemo ramani ya Sharifu Idrisi ya zamani, iliyochorwa na mtumishi wa kituo, na ushiriki wake kwenye kongamano la maandishi lililofanywa hivi karibuni katika chuo cha Allaamah Twabatwabai, kwa kushirikiana na jumuiya za kielimu za Iran katika mji mkuu wa Iran Tehran.

Sayyid Swafi amepongeza kazi iliyofanywa na kituo, ambayo iliwavutia watu wengi, akaashiria kuwa kikao hicho ni sehemu ya kuangalia mafanikio yaliyofikiwa kwenye kongamano hilo na kuangalia namna ya kuboresha kazi zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Muheshimiwa ametoa wito wa kuongeza juhudi ya kuboresha sekta ya uchoraji na maandishi, sambamba na umuhimu wa kufanya kongamano la kimataifa litakalo husisha wabobezi wa mambo ya jografia na turathi, kwa ajili ya kujadili mabadiliko yaliyotokea kwenye jografia, ambamo watu watanufaika na michoro ya Atabatu Abbasiyya pamoja na wataalam wake.

Sayyid Swafi akasisitiza kuwa umuhimu wa kushirikiana na sekta za kisekula kwa kufanya vikao vya pamoja na kubadilishana uzowefu wa kielimu, akasema kuwa mafanikio haya yanatokana na baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: