Wasimamizi wa uandaaji wa filamu hiyo ni kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel chini ya kitengo cha Habari.
Mtoaji wa filamu hiyo Sayyid Azharu Khamisi amesema “Filamu inaonyesha historia ya Qassim -a.s- katika zama za utawala wa bani Abbasi, imezinduliwa ndani ya malalo yake katika mji wa Hilla kufuatia kumbukumbu ya kifo chake (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Filamu imechezwa na raia wa Iraq, miongoni mwa watumishi wa kituo cha Alkafeel katika mji wa Jaswaan, imekubalika kwa kiwango kikubwa na wapenzi wa historia ya Ahlulbait (a.s)”.
Filamu hii ni kielelezo cha namna Atabatu Abbasiyya tukufu inavyojali na kuthamini ufundishaji wa historia ya Ahlulbait (a.s) kwa kutumia filamu.