Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya semina ya (Usomaji sahihi na hukumu za Tajwidi) katika wilaya ya Mashkhabu mkoani Najafu.
Kiongozi wa idara ya usomaji katika Maahadi ya Qur’ani tawi la Najafu chini ya Majmaa-Ilmi Sayyid Ahmadi Zaamili amesema “Semina hii ni miongoni mwa semina zinazofanywa na Maahadi kuanzia mwanzo wa mwaka katika maeneo tofauti ndani ya mkoa wa Najafu, zinalenga watu wa tabaka mbalimbali, kwa lengo la kuwafundisha usomaji sahihi, hukumu za tajwidi na mengineyo”.
Akaongeza kuwa “Semina ilikuwa na washiriki (30) wamefundishwa mihadhara miwili kwa wiki, wamesoma kwa vitendo na nadhariyya, ambapo wamesoma Qur’ani kwa kuzingatia hukumu na matamshi sahihi chini ya usimamizi wa Ustadh Abduridhwa Abudi”.
Hadi sasa tumeshafanya jumla ya semina (24) za Qur’ani tukufu katika mkoa wa Najafu na vitongoji vyake, zaidi ya wanafunzi (590) wameshiriki kwenye semina hizo.