Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imefanya kikao na wazazi wa wanafunzi wa shule ya awali ya Ahbaabul-Kafeel ambayo ipo chini yake.
Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema “Kikao kilikuwa na vipengele vingi, tumejadili mada tofauti kuhusu tabia za mabinti na namna ya kuwapa malezi bora”.
Akaongeza kuwa “Mkutano umejikita katika mada za kuwajenga wanafunzi na kuinua kiwango cha usomaji wa Qur’ani”.