Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kupitia Markazi Dirasaati Afriqiyya, kimejadili namna ya kushirikiana na Markazi Dirasaati Alkufa katika sekta ya elimu na tafiti.
Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema, “Tumempokea mkuu wa Markazi Dirasaati Alkufa ambayo ipo chini ya chuo kikuu cha Kufa Dokta Hasanaini Halo na ujumbe aliofuata nao, tumejadili kwa pamoja njia za kusaidiana na kushirikiana katika mambo ya kielimu na kitafiti”.
Katika mazungumzo yao, Muheshimiwa Shekhe Shimri amehimiza umuhimu wa kushirikiana na watafiti wa Markazi Dirasaati Alkufa, aidha wamesisitiza umuhimu wa kufanya program za kielimu kwa kushirikiana, kama vile nadwa na makongamano yanayohusu bara la Afrika.
Muheshimiwa akaeleza kazi inayofanywa na Markazi Dirasaati Afriqiyya katika bara la Afrika kwenye sekta ya elimu, utamaduni na huduma za kijamii, Markazi inaendelea kuwasiliana na maelfu ya wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika bara hilo.
Muheshimiwa Shekhe Shimri akaonyesha utayali wa Markazi kusaini makubaliano ya kushirikiana katika mambo yanayo husu raia wa Afrika waishio ndani na nje ya Iraq.
Naye mkuu wa Markazi Dirasaati Alkufa Dokta Hasanaini Halo, akatoa shukrani nyingi kwa uongozi wa Markazi Dirasaati Afriqiyya, kutokana na kazi kubwa wanayofanya ya kuimarisha uhusiano na taasisi za elimu katika mji wa Najafu kwa lengo la kuboresha ushirikiano katika sekta ya elimu na utafiti, akasisitiza umuhimu wa kuendelea kuwasiliana na kuendesha program kwa kushirikiana.