Idara ya Dini tawi la wanawake imetoa mihadhara ya kidini na kitamaduni kwa watumishi wa idara ya Zainabiyaati.

Idara ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, inatoa mihadhara ya kifiqhi na kimalezi kwa watumishi wa idara ya Zainabiyaati katika Atabatu Abbasiyya.

Kiongozi wa idara ya Dini bibi Adhraa Shami amesema “Idara imetoa mihadhara ya Fiqhi na Malezi kwa watumishi wa idara ya Zainabiyaati, sambamba na kuwafunisha hukumu za usomaji sahihi wa surat Fat-ha, chini ya ratiba ya uboreshaji iitwayo (Najielekeza kwa Abulfadhil)”.

Akaongeza kuwa “Muhadhara umetolewa katika Sardabu ya Alqami ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya utaratibu wa kushirikiana baina ya idara za wanawake kwa lengo la kutoa huduma bora kwa mazaairu watukufu”.

Akasisitiza kuwa “Nilazima mtumishi wa Ataba tukufu apambike kielimu na kimaadili, kwani wanafanya kazi sehemu takatifu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: