Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya nadwa kuhusu faharasi na faida yake kwa watumishi.
Nadwa imeratibiwa na kituo cha faharasi na taaluma katika mabtaba na Daaru-Mahtutwaat ya Atabatu Abbasiyya chini ya kitengo.
Mhadhiri wa Nadwa Sayyid Yahya Khadhiri amesema “Nadwa hii ni sehemu ya ratiba maalum inayotekelezwa na kituo kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi kuhusu mambo ya faharasi”.
Akaongeza kuwa “Program ya Faharasi inavipengele vikuu vinne, inalenga kujenga ushirikiano baina ya maktaba”.