Mawakibu zimekuja kutoa pole kwa bwana wa mashahidi Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na kufariki mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).
Mawakibu za waombolezaji zinakuja moja kwa moja kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kisha zinapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili na kuelekea katika malalo ya Imamu Hussein (a.s), kisha zinafanya Majlisi ya kuomboleza ndani ya malalo hiyo na kusoma tenzi na qaswida za kuomboleza.
Shekhe Zainul-Aabidina Al-Amiri mmoja wa watumishi wa Mawakibu amesema, “Wana Maukibu ya watoto wa Muslim bun Aqiil (a.s) wamezowea kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s), ikiwemo kifo cha mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu”.
Akaongeza kuwa “Tunatoa pole kwa Imamu wa zama (a.f), Maraajii watukufu na umma wa kiislamu, tutaendelea kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s) na kuhuisha ahadi ya kufuata mwenendo wao (a.s)”.
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa mkakati maalum wa kupokea mawakibu za waombolezaji, sambamba na kuandaa mimbari za kutolea mihadhara ya Dini na kufanya Majlisi za kuomboleza katika maeneo tofauti kwa ajili ya kubainisha yaliyotokea baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w).