Kitengo cha mahusiano kinatoa muhadhara kuhusu utamaduni kwa ugeni wa wanafunzi kutoka mji wa Qadisiyya

Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kimetoa muhadhara kuhusu utamaduni kwa ugeni wa wanafunzi kutoka umoja wa vijana wa Imamu Hussein (a.s) katika Mkoa wa Qadisiyya.

Muhadhiri Sayyid Jasaam Saidi amesema “Muhadhara umeeleza umuhimu wa utambulisho wa utamaduni na nafasi yake katika kulinda misingi ya jamii na maadili sambamba na njia za kulinda mmomonyoko wa maadili katika jamii”.

Akasema kuwa “Muhadhara umeeleza baadhi ya mavazi na uhusiano wake katika utamaduni na baadhi ya misingi kwenye elimu ya jamii, ambayo ni sehemu muhimu katika malezi ya jamii na familia”.

Katibu mkuu wa umoja wa vijana Sayyid Muntadhiru Albudairi, akashukuru Atabatu Abbasiyya kwa kuwapa mapokezi mazuri na kuwaandalia program bora zaidi, akaomba kudumisha mawasiliano baina ya wanafunzi na Ataba tukufu kwa lengo la kuwajenga kiitikadi na kitamaduni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: