Kituo cha utamaduni wa familia kwa kushirikiana na uongozi wa malezi katika mji wa Karbala wameandaa ratiba ya (uwanja wa utamaduni) kwa wanafunzi na walimu wa vituo vya kufuta ujinga.
Mkuu wa kituo bibi Sara Hafaari amesema “Program inalenga walimu na wanafunzi wa vituo vya kufuta ujinga kutoka kwenye vituo vya (Almiqaat, Adhwaa, Halima, Saadiyya na Mafaakhir)”.
Akaongeza kuwa “Program imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ikafuatiwa na muhadhara wenye anuani isemayo (Mbinu za kuamiliana na msukumo wa nafsi) iliyowasilishwa na mtoa nasaha Sundusi Muhammad, kukawa na kipengele cha vituo vya fikra kutoka kwa Bibi Kawakibu Abdusataar, kukawa na mashindano ya kimaarifa na kidini chini ya usimamizi wa Bibi Ikhlasu Jawaad”.
Akabainisha kuwa “Mwisho wa program hiyo kulikuwa na kipengele cha maswali na majibu, kilichopewa jina la (kutoka kwenu hadi kwenu) chini ya usimamizi wa Imaan Aun”.
Kituo kinafanya kila kiwezalo kuimarisha uhusiano na tabaka zote za jamii ya wanawake, kwa lengo la kutoa nasaha za kifamilia chini ya mwenendo wa Ahlulbait (a.s).