Chuo kikuu cha Alkafeel kimefanya kikao na wanafunzi wa kitivo cha udaktari, ambapo umetolewa muhadhara kuhusu (njia za utambuzi) kwa lengo la kuwajengea uwezo, ratiba hiyo imeratibiwa na kitengo cha ushauri nasaha hapo chuoni.
Mtoa mada alikuwa ni Sayyid Swafaa A’samu katika ukumbi wa kitivo cha famasia, ameeleza namna ya kutambua njia za utambuzi na kutumia kila njia wakati muwafaka.
Aidha amefafanua sifa za kila njia na namna ya kuitumia, kwa mfano kutumia njia ya utambuzi wa jamii katika kutatua matatizo ya jamii.
Kitengo kimejikita katika utoaji wa masomo ya ushauri nasaha, kwa lengo la kuinua uwezo wa wanafunzi kwenye sekta hiyo.