Sayyid Swafi amepokoe ugeni kutoka taasisi ya Daarul-Hadithi na amepongeza kazi yao ya kuhuisha vitabu vya riwaya.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amepokea ugeni kutoka taasisi ya Daarul-Hadithi iliyopo katika mji wa Qum (nchini Iran), amepongeza kazi yao ya kuhuisha vitabu vya riwaya.

Mkuu wa kituo cha tafiti za kiislamu na kimkakati chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Hashim Milani amesema “Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amepokea wageni kutoka taasisi ya Daarul-Hadithi, wakiongozwa na rais wa taasisi hiyo Sayyid Muhammad Kaadhim Twabatwabai, mkuu wa idara ya Akhlaq Shekhe Subhani Nayahi, mkuu wa machapisho ya Darul-Hadithi katika mji wa Qum”.

Akaongeza kuwa “Sayyid Swafi amepongeza kazi kubwa inayofanywa na taasisi hiyo ya kuhuisha vitabu vya riwaya, akasema kuwa yuko tayali kuendelea kutoa ushirikiano katika uchapishaji wa vitabu vya hadithi, turathi na vinginevyo sambamba na kutafsiri vinavyo hitaji kutafsiriwa, aidha amesema kuwa Atabatu Abbasiyya ikotayali kuchapisha kitabu cha (Manlaa Yahdhuruhul-Faqiihi) na kitabu cha (Nahjul-Balagha), na vitabu vingine vitakavyofanyiwa uhakiki na Daarul-Hadithi”.

Akafafanua kuwa “Katika kikao hicho wameongea pia umuhimu wa kujali hauza na turathi za wanachuoni, sambamba na kufungamanisha taasisi na vituo vya tafiti chini ya Maraajii watukufu ili kuweka usalama wa kazi, na kuwepo kwa uzito wa mambo ya kifiqhi”.

Akabainisha kuwa “Wageni wamesema kuwa wanaendelea kufanyia kazi vitabu vyote vilivyoandikwa na Shekhe Swaduqu, aidha wamesema kuwa wanatarajia kumaliza kufanya uhakiki wa kitabu cha Nahjul-Balagha mwaka kesho”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: