Wahudumu wa Ataba mbili wanaomboleza kifo cha Bibi Zaharaa (a.s).

Wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wameomboleza kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu kupitia maukibu ya pamoja.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, ameshiriki kwenye maukibu hiyo pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo bila kusahau kundi la mazuwaru watukufu.

Sayyid Badri Mamitha kutoka idara ya Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya amesema “Maukibu imeanza matembezi kutokea ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wakiimba qaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia za majonzi na huzuni katika nyoyo za waumini, wakaenda hadi kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Maukibu ilipofika kwenye malalo ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s) ikafanya Majlisi ya kuomboleza iliyopambwa na kaswida na tenzi zilizo eleza dhulma aliyofanyiwa bibi Zaharaa (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: