Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kimefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu.
Majlisi imepambwa na muhadhara uliojikita katika kueleza dhulma aliyofanyiwa Bibi Zaharaa (a.s) na yaliyotokea baada ya kifo cha baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), sambamba na msimamo wake wa kutetea bendera ya Utume na Uimamu.
Majlisi imehudhuriwa na rais wa kitengo na watumishi wengine, ikahitimishwa kwa qaswida na tenzi za kuomboleza katika mazingira yaliyojaa majonzi na huzuni.
Kufanya kumbukumbu za matukio ya kidini ni sehemu ya ratiba maalum iliyoandaliwa na kitengo hiki kwa ajili ya kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s).