Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya, kimetoa wito kwa waandishi washiriki kwenye mradi wa (Qalamul-Walaa) unaolenga kuandika utukufu wa Ahlulbait (a.s).
Kituo kimetoa wito wa kuandika kuhusu Bibi Zaharaa (a.s) kama sehemu ya kushiriki katika kutunza visa na hekaya kwa kuandika michoro inayo onyesha turathi za Ahlulbait (a.s).
Washindi watatangazwa kupitia mitandao ya kituo cha utamaduni wa familia.
Kwa kila anaetaka kushiriki ajiunge kwenye kundi kupitia link ifuatayo: https://t.me/muntada313