Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya mtihani wa nadhariyya kwa wanafunzi walioshiriki kwenye semina ya usomaji sahihi na hukumu za usomaji (Ahkaamu-Tilaawah).
Waliopewa mtihani ni wanafunzi wa hatua ya kwanza katika Maahadi ya Qur’ani tukufu mjini Najafu, tawi la wilaya ya Hamza mashariki chini ya Majmaa.
Mkuu wa tawi hilo Sayyid Bahaa Tamimi amesema “Tumewapa mtihani kwa ajili ya kutambua viwango vya wanafunzi na uwelewa wao katika masomo waliyo fundishwa siku za nyuma, sambamba na kuona kama wanaweza kuendelea hatua ya mbele, kwani wanatakiwa kukuza uwezo wao katika fani ya usomaji na kujiandaa kushiriki kwenye mashindano ya Qur’ani ambayo hufanywa katika ngazi ya wilaya hadi taifa”.
Akaongeza kuwa “Zaidi ya wanafunzi (20) miongoni mwa wakazi wa wilaya hii wameshiriki kwenye semina hiyo, iliyodumu kwa muda wa miezi miwili chini ya Ustadh Muhammad Nabiil Jawaad, walikuwa wanapewa mihadhara mitatu kwa wiki”.