Idara ya shule za Alkafeel imefanya kikao cha kujadili maandalizi ya kongamano la (Ruuhu-Nnubuwwah) la kimataifa awamu ya sita.
Kikao hicho kimehudhuriwa na rais wa kamati ya maandalizi Bibi Bushra Jabaar Alkinani, kimejikita katika kujadili ratiba ya kongamano.
Kamati ya maandalizi imeagizwa kuratibu mambo vizuri na kutatua changamoto zote zinazoweza kujitokeza.
Maandalizi yanaendelea vizuri kufatia kukaribia kufanyika kwa kongamano hilo.
Ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa vikao vya maandalizi ambapo wajumbe wanapeana maelekezo na kubadilishana uzowefu.