Qawaaidu-Rijaali.. chapisho jipya lutolewa na kitengo cha maarifa.

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimechapisha kitabu cha (Qawaaidu-Rijaali).

Wasimamizi wa uchapaji wa kitabu hicho ni idara ya kusimamia maarifa chini ya kitengo, nacho ni risachi za misingi ya Ilmu-Rijaali kutoka kwenye mihadhara ya Sayyid Ahmadi Husseini Aljawaadi.

Kitabu hicho kina kurasa (500) zenye sehemu kuu tatu.

Utangulizi unafafanua kuhusu (Ilmu-Rijaali) na umuhimu wake, kisha mtunzi akaandika kuhusu vigawanyo vya Habari, halafu sehemu ya pili akaandika uzingatiaji wa Habari na usahihi wake, sehemu ya tatu akaandika Habari isiyozingatiwa na udhaifu wake.

Tambua kuwa idara ya maarifa imeshachapisha vitabu vingi, aidha huratibu nadwa mbalimbali za kielimu, inamchango mkubwa kwenye kongamano la kimataifa la turathi za kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: