Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimeomboleza kifo cha Bibi Zaharaa (a.s) katika nchi ya Chadi kwa mujibu wa riwaya ya tatu.
Kiongozi wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema “Mubalighina wa Markazi kwenye nchi tofauti za Afrika wamefanya Majlisi za kuomboleza kifo cha Bibi Fatuma (a.s) kupitia ratiba ya kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Mubalighi wa Markazi katika nchi ya Chadi Dokta Ali Muhammad amesema, wameshiriki wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) kwenye Majlisi hiyo”.
Akafafanua kuwa “Majlisi imepambwa na muhadhara kuhusu Maisha ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na utukufu wake, Pamoja na kueleza dhulma aliyofanyiwa na athari yake katika Dini na jamii ya wakati ule”.