Wahudumu wa Atabatu Abbasiyya hufanya tukio la kiibada katika siku ya Jumanne na Alkhamisi ya kila wiki, limefunguliwa kwa kusoma ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) iliyofuatiwa na wimbo wa (Lahnul-Ibaa) wakiwa wamesimama mbele ya kaburi takatifu.
Tukio hilo limefanywa mbele ya mlango wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na kundi kubwa la mazuwaru na wageni wa Atabatu Abbasiyya tukufu.