Kitengo cha habari na utamaduni kimeomboleza kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) nchini Tanzania.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimeomboleza kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu, kwa kufanya Majlisi ya kuomboleza nchini Tanzania.

Majlisi imefanywa mkoani Kigoma nchini Tanzania, Mkuu wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema “Majlisi imehudhuriwa na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) chini ya usimamizi wa mubalighi wa Markazi Shekhe Ammaari Maulidi”.

Akaongeza kuwa “Majlisi imepambwa na muhadhara kuhusu Maisha ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na nafasi yake mbele ya baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na namna alivyo pambana katika kutetea bendera ya Utume na Uimamu, alikuwa ni mtetezi wa baba yake na mume wake”.

Markazi Dirasaati Afriqiyya huratibu program za kiibada na kitablighi katika bara la Afrika sambamba na kuendesha harakati za kitamaduni, kibinaadamu na kijamii kwa faida ya maelfu ya raia wa Afrika na wafuasi wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: