Idara ya Fatuma binti Asadi katika Atabatu Abbasiyya, imekamilisha maandalizi ya mtihani wa muhula wa kwanza.
Kiongozi wa idara bibi Fatuma Mussawi amesema “Idara imekamilisha maandalizi ya kufanya mtihani wa muhula wa kwanza katika mwaka huu wa masomo”.
Akaongeza “Tumeunda kamati ya walimu wanne kwa ajili ya kupitia maswali kabla ya kuanza mtihani”, akasema “Wanafunzi wanatakiwa kufuata ratiba ya mitihani itakayo anza siku ya Jumamosi ya tarehe (23/12/2023) hadi tarehe (10/1/2024)”.
Akasisitiza kuwa wanafunzi wanatakiwa kufuata maelekezo yaliyotolewa siku za nyuma, na akawatakia mafanikio mema katika safari ya kutafuta elimu.