Ameyasema hayo alipokutana na ugeni wa mubalighina wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na wajumbe wa hauza ya Najafu akiwepo rais wa kitengo cha Dini Shekhe Swalahu Karbalai.
Sayyid Swafi amesema “Mazuwaru wa Ataba tukufu wanahaja kubwa ya mubalighina kwa moja ya mambo mawili, kuuliza swali moja kwa moja au kuhitaji ufafanuzi wa kisheria na maelekezo katika jambo la kijamii, kwani wanakuangalieni kwa jicho la mnasihi”.
Akaongeza kuwa “Ni wazi kuwa muulizaji wakati mwingine anaweza kuja kukiri dhambi zake, hapo unatakiwa kumpa muongozo wa namna ya kufanya toba, hakika mlango wa toba uko wazi na nyie mnatambua vizuri jambo hilo”.
Akasisitiza mambo mawili: Umuhimu wa mafunzo ya kiislamu kwa uwazi na umuhimu wa kupambika na maadili mema yanayojenga uaminifu kwa zaairu, mnatakiwa kuiga mwenendo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kizazi chake kitakasifu (a.s).
Rais wa kitengo cha Dini Shekhe Swalahu Karbalai amesema “Sayyid Swafi amepokea ugeni wa mubalighina kutoka Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, ametoa nasaha na maelekezo ya namna ya kuhudumia mazuwaru watukufu”.
Akaongeza kuwa “Sayyid Swafi ametoa nasaha kuhusu umuhimu wa Tablighi kwa mazuwaru na kufanya kila kinachowezekana kuhakikisha zaairu anafikia malengo yake”.