Majmaa inafanya mitihani ya mwisho kwa wanafunzi wa semina za hukumu za usomaji na tajwidi katika mji wa Baabil.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imetoa mitihani ya mwisho kwa wanafunzi walioshiriki kwenye semina za hukumu za usomaji na tajwidi katika mji wa Baabil.

Kiongozi wa tawi la Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Baabil Sayyid Muntadhiru Mashaikhi amesema “Wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa zaidi ya (250) miongoni mwa walioshiriki kwenye semina za Qur’ani, ambapo walifundhishwa Tafsiri, Uluumul-Qur’ani, Kusimama na kuanza, Sauti na Naghma”.

Akaongeza kuwa “Mitihani itadumu kwa siku nne, wanafanya mitihani ya nadhariyya na vitendo kwa kufuata ratiba iliyoandaliwa”.

Akabainisha kuwa “Mradi unahatua tatu zenye viwango tofauti, masomo yake hudumu kwa muda wa miaka miwili”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: