Hivi karibuni kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimechapisha juzuu la kwanza la kitabu la (wadau wa Islahi kwa Imamiyya katika ulimwengu wa kiislamu wa sasa).
Wasimamizi wa uchapishwaji wa kitabu hicho ni kituo cha tafiti za kiislamu chini ya kitengo, mtunzi wa kitabu ni Sayyid Hashim Almilani.
Kitabu kimeandika tafiti za msingi kuhusu masomo ya Dini pamoja na mambo mapya na kujibu changamoto kwa lengo la kupata uhakika.
Kitabu kimejikita katika kueleza mambo muhimu kuhusu wadau wa islahi kwa Imamiyya, na kutaja mambo muhimu katika mtazamo wa Dini na mahitaji ya zama hizi sambamba na kueleza utamaduni wa kiislamu dhidi ya mitazamo tofauti inayozuka.