Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefungua kisima kipya katika nchi ya Tanzania kupitia mradi wa Mnyweshaji wenye kiu Karbala (Saaqi Atwaasha Karbalaa).
Wasimamizi wa mradi huo ni Markazi Dirasaati Afriqiyya.
Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema “Markazi imefungua kisima kipya Tanzania kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Bibi Zaharaa (a.s), kama sehemu ya mradi wa Markazi wa kuchimba visima katika nchi tofauti za Afrika unaoitwa (Saaqi Atwaasha Karbalaa)”.
Akaongeza kuwa “Hadi sasa tunazaidi ya visima ishirini vilivyo chimbwa kupitia mradi huu, unaolenga kutoa huduma za kibinaadamu katika jamii ya waafrika ambao wanatatizo kubwa la upungufu wa maji”.
Akabainisha kuwa “Markazi inaendelea na mradi huo kwenye nchi zaidi ya (13) za Afrika, akasema kuwa kuna visima vingine vinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni”.