Jumuiya ya Al-Ameed imefanya kikao cha kujadili maandalizi ya kongamano la uwezo wa vijana kitaifa.

Jumuiya ya Al-Ameed imefanya kikao cha kujadili maandalizi ya kongamano la uwezo wa vijana katika taifa, mada za kongamano zimejikita katika kueleza misingi ya Maisha bora.

Wamejadili miradi ya kielimu ikiwa ni pamoja na uwezo wa vijana katika taifa, uchambuzi wa misingi ya Maisha bora kwa mujibu wa tafiti za kielimu.

Katika kikao hicho wamejadili pia ushirikiano baina ya Jumuiya ya Al-Ameed na chuo kikuu cha Alqadisiyya na kufanya kongamano la kielimu kwa Pamoja, sambamba na kuimarisha uhusiano baina ya Jumuiya na taasisi zingine za kielimu.

Wajumbe wakaongea kuhusu mradi wa mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) na kongamano la Imamu Hassan (a.s) la kimataifa awamu ya kumi na moja, kuhusu kubadili tarehe ya kongamano hilo na kutoa fursa zaidi kwa watafiti, sambamba na kujadili miradi mingine iliyofanywa na inayotarajiwa kufanywa na vitengo tofauti vya Jumuiya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: