Rais wa kitengo Dokta Muhammad Hussein Jaabir amesema “Mtihani wa awamu ya tatu kwa watumishi wa zamani umehusisha zaidi ya watu 150, utadumu kwa muda wa siku tatu”.
Akaongeza kuwa “Wanapewa mtihani kisha wanahojiwa mbele ya kamati maalum kupima uwelewa wao na kuangalia njia bora ya kuwajengea uwezo”.
Akafafanua kuwa “Kitengo chetu kinafanya kila kiwezalo katika kuboresha uwezo na vipaji vya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.