Atabatu Abbasiyya imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s).

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya, imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mhadhiri wa Majlisi hiyo Sayyid Mustwafa Shibri amesema “Kama kawaida ya Atabatu Abbasiyya katika kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s) likiwemo hili la kifo cha Ummul-Banina (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Muhadhara umejikita katika kueleza historia ya Ummul-Banina (a.s) na msimamo wake”.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum katika kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s) ikiwa ni pamoja na ratiba za uombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: