Makamo rais wa kitengo Shekhe Zainul-Aabidina Kuraishi amesema “Baada ya kumaliza msimu wa huzuni za Fatuma kwa mujibu wa riwaya ya tatu, watumishi wa kitengo chetu wameweka mapambo meusi yanayo ashiria huzuni kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Ummul-Banina (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Mabango na vitambaa vya ukubwa tofauti vimewekwa kila sehemu katika malalo ya Abulfadhil na maeneo yanayo zunguka haram”.
Akaendelea kusema “Atabatu Abbasiyya inaomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) kwa kuandaa ratiba kamili, inayojumuisha ufanyaji wa Majlisi za kuomboleza na kujata historia yake takatifu (a.s)”.