Atabatu Abbasiyya tukufu imeomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) kwa kufanya Majlisi ndani ya haram tukufu.
Majlisi imeandaliwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya.
Mzungumzaji alikuwa ni Shekhe Swahibu Twaiy, ameongea historia ya Ummul-Banina (a.s) na akabainisha mambo muhimu aliyofanya katika Maisha yake, kama kuwalea maimamu wawili Hassan na Hussein (a.s), namna alivyo jitolea kwa Imamu Hussein (a.s) katika vita ya Twafu.
Katika Majlisi hiyo ameshiriki muimbaji mashuhuri Baasim Karbalai kwa kusoma kaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia ya majonsi na huzuni katika nyoyo za wapenzi wa Ahlulbait (a.s).
Majlisi zitaendelea kufanywa ndani ya harama ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa muda wa siku nne baada ya swala ya Magharibi na Isha.