Kwa kumbukumbu ya kifo chake.. idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake yakumbuka historia ya Maisha ya Ummul-Banina (a.s).

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na Markazi Swidiqatu-Twahirah (a.s) imekumbuka historia ya Maisha ya Ummul-Banina (a.s) kwa kufanya Majlisi ya kuomboleza kifo chake.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha ikasomwa ziara ya Ummul-Banina (a.s) halafu ukafuata muhadhara wenye anuani isemayo (Ummul-Banina mtambuzi), ambapo imezungumzwa historia ya Maisha yake.

Likafuata igizo liitwalo (Mama wa uaminifu na watoto wake wanne), limeonyesha mafungamano ya Imamu Hujjah (a.f), mazingira ya Ummu Salama na riwaya ya Turbah itakapo badilika kuwa damu baada ya kuuwawa Imamu Hussein (a.s), Pamoja na mazingira ya muili wa mwisho kuwasiri Madina kutoka katika msafara wa Zainabu, na kupewa taarifa Ummul-Banina ya kifo cha Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake Pamoja na watoto wake wanne, igizo limepambwa na qaswida ya kuomboleza msiba wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: