Kuhitimisha ratiba ya wiki ya kuwajengea uwezo watumishi.

Kamati imekamilisha ratiba maalum ya wiki ya kuwajengea uwezo watumishi wa Atabatu Abbasiyya.

Ratiba hiyo inasimamiwa na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Ataba.

Rais wa kitengo Dokta Muhammad Hassan Jaabir amesema “Ratiba ilikuwa na vipengele tofauti vya Dini, Utamaduni, Mapumziko, Mashindano pamoja na kutembelea miradi ya Ataba tukufu, tunaendelea kuandaa ratiba zaidi kwa ajili ya kuboresha uwezo wa watumishi wa Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa “Siku ya mwisho ya ratiba hii ni maalum kwa kusikiliza maoni ya watumishi, tunapokea maoni yao na kuyafikisha kwenye uongozi wa juu kwa ajili ya kufanyiwa kazi, kwa ujumla maoni yote ni mazuri”.

Akabainisha kuwa “Lengo kuu la ratiba hii ni kudumisha mawasiliano na ushirikiano baina ya watumishi na kuwafanya waache kufanya kazi kwa mazowea, waelewe harakazi za sekta ya viwanda, kilimo, malezi, utumishi na shughuli zingine zinazofanywa na Ataba tukufu sambamba na kuongeza ufanisi katika sekta zao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: