Ugeni wa Atabatu Abbasiyya umefika katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad kwa ajili ya kufanya kongamano la wanawake kwa mara ya kwanza chini ya kauli mbiu isemayo (Bibi Fatuma kigezo chetu).
Ugeni wa Ataba unaongezwa na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami, rais wa kitengo cha Dini Shekhe Swalahu Karbalai, makamo rais wa kitengo cha mahusiano Sayyid Muhammad Jalukhani na baadhi ya viongozi wa Ataba.
Baada ya kuwasili wamekutana na kamati ya wenyeji chini ya chuo cha Alkauthar na wamejadili ratiba ya kongamano na maandalizi yake.
Kongamano litafanywa kwa mara ya kwanza kwa kushirikiana na chuo cha Alkathar katika mji mkuu wa Pakistani Islamabad, kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kuanzia tarehe 29/12/2023 na litadumu kwa muda wa siku tatu.
Kongamano litakuwa na vipengele tofauti, kutakuwa na kipengele cha ufunguzi, halfa ya waliofikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria, uwasilishaji wa mada kuhusu historia ya Fatuma Zaharaa (a.s), maonyesho ya kazi zinazofanywa na wanawake na maonyesho ya vifaa vya watoto na mengineyo.